Login | Register

Sauti za Kuimba

Twendeni Mezani Mwake Lyrics

TWENDENI MEZANI MWAKE

Twende wote mezani mwake
Tukale mwili na kuinywa damu
Ametualika Bwana Yesu kwa karamu

 1. Yesu mwili na damu, chakula safi
  Kishibishacho roho zetu
  Twendeni sote tukampokee ametualika
 2. Mimi ndicho chakula cha kushibisha
  Kilichoshuka kwake Baba
  Anayenila ataishi vema siku zote
 3. Alaye chakula kwa kustahili
  Hukaa ndani yangu mimi
  Nami ndani yake siku zote asema Bwana
Twendeni Mezani Mwake
CHOIR
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments