Twendeni Tuingie Kwake
| Twendeni Tuingie Kwake | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Views | 7,027 | 
Twendeni Tuingie Kwake Lyrics
- { Twendeni tuingie kwake
 Na nyimbo nzuri za shangwe } *2
- Dunia nzima imshangilie Bwana
 Kwa furaha tumtumikie wote
 Tumwendee na nyimbo za shangwe
- Mjue Bwana wetu ni Mungu
 Ametufanya na tuko watu wake
 Sisi kondoo wa malisho yake
- Ingieni mlangoni kwa kumsifu
 Nyumbani mwake tumtolee heshima
 Tutukuze jina lake kubwa mno
- Kweli Mungu kwa Baba mwenyezi
 Na kwa mwana Mwokozi wetu
 Na kwa Roho Mtakatifu ndani mwetu
 
  
         
                            