Umekosa Nini Yesu
| Umekosa Nini Yesu | |
|---|---|
| Alt Title | Njia ya Msalaba | 
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 58,700 | 
Umekosa Nini Yesu Lyrics
- Tuifuate Njia ya Msalaba, tuifuate mpaka Kalvari
 Tusimamapo bila haya, (msalaba *2) huponya roho
 * * * * * *
- Umekosa Nini we Yesu, kushtakiwa bure kwa Pilato
 Wenye kustahili hukumu, si wewe, si wewe, Bwana ni sisi
- Ole msalaba huo mzito, apagazwa Mwana Mpenzi wa Mungu
 Mwili waenea mateso, alipa, alipa madhambi yetu
- Ona Mumba Mbingu na nchi, yupo chini mzigo wamwelemea
 Na mtu kiumbe chake kwa ukali, ampiga, ampiga bila huruma
- Huko njiani we Maria, waonaje hali ya mwanao
 Ni damu tupu na vidonda, machozi, machozi yamfumba macho
- Kwa Simoni heri ya kweli, mimi pia Yesu nisaidie
 Kuchukua mzigo wa ukombozi, kuteswa, kuteswa pamoja nawe
- Uso wa Yesu malaika, Bethlehemu wakuabudu
 Bahati yake Veronika, kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu
- Wakimvuta huku na huku, wauaji wakamchokesha bure
 Chini wamtupa bado kwa nguvu, aibu, aibu yao milele
- Wanawake wa Israeli, msilie kwa sababu hiyo
 Muwalilie hao kwa dhambi, upanga, upanga ni juu yao
- Mwokozi sasa ni ya tatu, kuanguka chini ya msalaba
 Katika dhambi za ulegevu, nijue, nijue kutubu hima
- Muje malaika wa Mbingu, funikeni mwiliwe kwa huruma
 Vidonda vyake na utupu, askari, askari wamvulia
- Hapo mkristu ushike moyo, Bwana wako alazwa msalabani
 Mara miguu na mikono, yafungwa, yafungwa kwa misumari
- Yesu mpenzi nakuabudu, msalabani unapohangaika
 Nchi yatetemeka kwa hofu, na jua, na jua linafifia
- Mama Maria mtakatifu, upokee maiti ya mwanao
 Tumemwua kwa dhambi zetu, twatubu, twatubu kwake na kwako
- Pamoja naye kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo
 Yesu tuwe wakristu wa kweli, twakupa, twakupa sasa mapendo
 * * * * * * * * *
- Katika roho yangu Bwana, chora mateso niliyokutesa
 Nisiyasahau madeni, na kazi, na kazi ya kuokoa
 
  
         
                            