Uniondolee Dhambi Nitakase
| Uniondolee Dhambi Nitakase | |
|---|---|
|  | |
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Video | Watch on YouTube | 
| Views | 47,375 | 
Uniondolee Dhambi Nitakase Lyrics
- Uniondolee dhambi, nitakase,
 Unioshe niwe mweupe pe *2
- Nakiri makosa yangu, naziona dhambi zangu
 Unioshe niwe mweupe pe
- Mimi kweli mkosefu, tangu kuzaliwa kwangu
 Mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu
- Hivyo unafanya vyema, wewe unaponihukumi
 Una haki unaponiadhibu
- Wewe wataka unyofu, ule unyofu wa ndani
 Nifundishe hekima moyoni
- Niumbie moyo safi, na uweke ndani yangu,
 Roho mpya iliyo thabiti.
 
  
         
                            