Huniongoza Mwokozi

Huniongoza Mwokozi
Performed bySauti Tamu Melodies
AlbumNyimbo za Sifa
CategoryGeneral
Composer(traditional)
VideoWatch on YouTube
Views54,435

Huniongoza Mwokozi Lyrics

  1. Huniongoza Mwokozi,
    ndipo nami hufurahi
    Niendapo pote napo,
    ataniongoza papo

    Huongoza, hunishika kwa mkono wa hakika
    Nitaandamana naye Kristu aniongozaye

  2. Pengine ni mashakani,
    nami pengine rahani
    Ni radhi ijayo yote,
    yupo nami siku zote
  3. Mkono akinishika,
    kamwe sitanung`unika
    Atachoniletea,
    ni tayari kupokea
  4. Nikiishika kazi chini,
    nitakwenda nako mbinguni
    Nako nitamtukuza,
    Kristu aliyeongoza