Univishe Pete

Univishe Pete
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMilele Milele Msifuni (Vol 1)
CategoryHarusi
ComposerA. K. C. Singombe
Views3,008

Univishe Pete Lyrics

 1. { Ewe mwenzangu univishe pete kwenye chanda changu,
  Iwe ni alama ya uaminifu wako } *2

 2. Naapa mbele ya Mungu, mimi ni wako siku zote,
  Nitamuacha Baba nitamwacha na mama
  Niambatane nawe, nasi tutakuwa mwili mmoja
 3. Wewe sio malaika ni mwanadamu kama mimi,
  Makosa kawaida tuko sawa maumbile
  Maumbile ya Mungu, nitakusamehe ukinikosea
 4. Macho yangu yameona, yameona wengi sana,
  Kati yao wengi, ninakuvika pete
  Iwe alama yangu ya uaminifu wangu kwako