Login | Register

Sauti za Kuimba

Upendo Lyrics

UPENDO

 1. Bwana Yesu - alituachia amri moja
  Amri ile kuu (upendo)
  Alisema - nawapa - amri yangu ni hii
  nyinyi mpendane (pendaneni)

  Pendo [pendo lake] la Bwana
  ni pendo la kweli, upendo ule wa Roho,
  Ndugu kweli tupendane, upendo ule Bwana

 2. Pendo hilo - la Bwana - ni upendo ule
  usio nao wivu (na wivu)
  Ndilo pendo - la kweli - ni upendo ule
  wenye uvumilivu (na kweli)
 3. Tupendane - sisi - sote upendo ule
  usio na chuki (na tuku)
  Tukumbuke - kwamba - upendo wa kweli
  hauna utengano (tengano)
 4. Enyi ndugu - zangu tu - tutimize amri
  ile tuliyopewa (na Bwana)
  Tuonyeshe - watu - ule upendo
  tuliopewa na Bwana (Mwokozi)
Upendo
CHOIR
CATEGORYLove
 • Comments