Utukufu (MIGORI)

Utukufu (MIGORI)
ChoirSt. Joseph Migori
AlbumUzuri wa Yesu
CategoryTBA

Utukufu (MIGORI) Lyrics

 1. Utukufu kwa Mungu juu
  Na amani duniani
  Na amani kwa watu wote
  {Wenye - wenye mapenzi,
  Watu - wenye mapenzi
  Mema - wenye mapenzi
  Watu - wenye mapenzi mema }*2

 2. Tunakusifu tunakuheshimu
  Tunakuabudu tunakutukuza
  Tunakushukuru kwa ajili ya
  Utukufu wako, wako mkuu
 3. Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni,
  Mungu Baba mwenyezi ee Bwana Yesu Kristu
  Mwana wa pekee ee mwana Mungu
  Mwanakondoo wa Mungu, mwana wa Baba
 4. Mwenye kuondoa dhambi za dunia
  Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia
  Pokea ombi letu ewe mwenye kuketi
  Kuume kwa Baba, utuhurumie
 5. Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako
  Peke yako mkuu ee Bwana Yesu Kristu
  Pamoja na roho mtakatifu
  Katika utukufu, wa Mungu Baba amina