Utukufu (MISA MWANDA)
Utukufu (MISA MWANDA) |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 4,827 |
Utukufu (MISA MWANDA) Lyrics
- Utukufu kwa Mungu juu
Na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema
Mungu tunakusifu
Mungu tunakuheshimu
Mungu tunakuabudu, tunakutukuza
- Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu
Ee Bwana Mungu, mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba mwenyezi
- Ee Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee,
Ee Bwana Mungu,
mwana kondoo wa Mungu mwana wa Baba
- Mwenye kuondoa dhambi za dunia, utuhurumie
Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia,
pokea ombi letu
- Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie,
Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako mtakatifu
Peke yako Bwana peke yako mkuu Yesu Kristu
- Pamoja na roho mtakatifu
Katika utukufu wa Mungu Baba amina.