Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI)
| Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI) |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 50,640 |
Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI) Lyrics
Utukufu juu kwa Mungu, Utukufu juu Mbinguni
Na amani kote duniani, Kwa wenye mapenzi mema
- Tunakusifu tunakuheshimu, tunakuabu tunakutukuza
Twakushukuru kwa ajili, ya utukufu wako mkuu
- Ewe Mungu ndiye mfalme, wa mbinguni Baba mwenyezi
Ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee mwana wa baba
- Ewe Yesu mwanakondoo, wa Mungu mwana wa Baba
Ewe mwenye kuziondoa, dhambi zetu tuhurumie
- Ewe mwenye kuziondoa, za dunia dhambi za watu
Ewe mwenye rehema nyingi, upokee maombi yetu
- Uketiye kuume kwake, Mungu Baba tuhurumie
Kwa kuwa ndiwe uliye, peke yako Mtakatifu
- Peke yako ni wewe Bwana, peke yako Bwana mkuu
Peke yako ni mkombozi, peke yako Yesu Kristu
- Naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake
Mungu mmoja anayeishi, na kutawala milele yote.