Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI)

Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI)
ChoirTBA
CategoryTBA

Utukufu Juu kwa Mungu (MISA KARIOBANGI) Lyrics

Utukufu juu kwa Mungu, Utukufu juu Mbinguni
Na amani kote duniani, Kwa wenye mapenzi mema

 1. Tunakusifu tunakuheshimu, tunakuabu tunakutukuza
  Twakushukuru kwa ajili, ya utukufu wako mkuu
 2. Ewe Mungu ndiye mfalme, wa mbinguni Baba mwenyezi
  Ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee mwana wa baba
 3. Ewe Yesu mwanakondoo, wa Mungu mwana wa Baba
  Ewe mwenye kuziondoa, dhambi zetu tuhurumie
 4. Ewe mwenye kuziondoa, za dunia dhambi za watu
  Ewe mwenye rehema nyingi, upokee maombi yetu
 5. Uketiye kuume kwake, Mungu Baba tuhurumie
  Kwa kuwa ndiwe uliye, peke yako Mtakatifu
 6. Peke yako ni wewe Bwana, peke yako Bwana mkuu
  Peke yako ni mkombozi, peke yako Yesu Kristu
 7. Naye Roho Mtakatifu, katika utukufu wake
  Mungu mmoja anayeishi, na kutawala milele yote.

Favorite Catholic Skiza Tunes