Utukufu Juu Kwa Mungu
Utukufu Juu Kwa Mungu |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 20,130 |
Utukufu Juu Kwa Mungu Lyrics
- Utukufu juu kwa Mungu, na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi, kwa
watu wenye mapenzi mema
Wenye mapenzi mema
Tunakusifu [Bwana] tunakuheshimu
Tunakuabudu tunakuabudu
Bwana tunakutukuza
- Tunakushukuru Mungu kwa ajili
Ya utukufu wako mkuu
E Bwana ndiwe Mungu Mfalme wa milele
- E Mwenyezi Mungu Baba Ewe Bwana Yesu Kristu
Mwana wa pekee wa Mungu,
Mwanakondoo wa Mungu, Mwana wake Baba
- Unayeondoa dhambi, dhambi zote za dunia
Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie
Pokea ombi letu
- Mwenye kuketi kuume kuume kwake Mungu Baba
Bwana utuhurumie, pekee yako Bwana
Ndiwe mtakatifu
- Pekee yako ndiwe Bwana, pekee yako mkuu
Ee Bwana Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu
Milele na milele