Utukufu Kwa Mungu
| Utukufu Kwa Mungu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 24,239 |
Utukufu Kwa Mungu Lyrics
- Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Tunakusifu tunakuheshimu
Tunakuabudu tunakutukuza.
- Tunakushukuru Mungu kwa ajili
Ya utukufu wako mkuu, Ee Bwana ni Mungu
Ndiwe mfalme wa mbinguni.
- Ee Baba mwenyezi Bwana Yesu Kristu
Ee mwana wa pekee ee Mungu Mwanakondoo
Wa Mungu mwana wake Baba
- Mwenye kuondoa dhambi za dunia
Utuhurumie, tuhurumie maombi yetu
Bwana uyapokee
- Mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie
Kwa kuwa ndiwe peke yako ni Mtakatifu
- Peke yako Bwana peke yako mkuu
Ewe Yesu Kristu, Pamoja naye Roho Mtakatifu
Milele yote.