Utukufu Kwa Mungu
Utukufu Kwa Mungu |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 5,518 |
Utukufu Kwa Mungu Lyrics
- Utukufu kwa Mungu, na amani duniani
Kwa watu wenye mapenzi mema
Kwa wenye mapenzi mema
- Tunakusifu Bwana tunakuheshimu
Twakuabudu Bwana tunakutukuza
Twakushukuru Baba Mwenyezi mfalme wa Mbinguni
- Ewe Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee
Mwanakondoo wa Mungu, mwana wake Baba
Uondoaye makosa yetu tuhurumie
- Tunakusifu Bwana utusikilize
Wewe unayeketi kuume kwa Baba
Ni pekee Bwana ni mtakatifu mkuu Yesu Kristu
- Pamoja naye Mungu, Roho Mtakatifu
Katika utukufu wake Mungu Baba
Milele yote milele yote amina amina