Jipeni Moyo Msiogope

Jipeni Moyo Msiogope
Alt TitleWaambieni Watu
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumHodi Hodi
CategoryMajilio (Advent)
ComposerAlfred Ossonga
Views9,160

Jipeni Moyo Msiogope Lyrics

  1. Waambieni watu walio na moyo wa hofu *2
    { Jipeni moyo, msiogope (ogope) [kwa maana]
    Tazama Mungu wenu nakuja kuwaokoa nyinyi } *2

  2. Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu
    (Na fanyeni imara magoti yaliyolegea *2)
  3. Ndipo macho ya vipofu yatafunguliwa
    (Na masikio ya viziwi yatazinduliwa *2)
  4. Ndipo na kilema atarukaruka
    (Na ulimi wake bubu ndipo utakapoimba *2)
  5. Na katika nyika maji yatabubujika,
    (Na nchi yenye kiu itakuwa chemichemi *2)