Watoto wa Mayahudi
| Watoto wa Mayahudi | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 6,220 | 
Watoto wa Mayahudi Lyrics
- Watoto wa Mayahudi walimlaki Bwana
 Wakiyachukua matawi ya mizeituni
 Wakipiga kelele wakisema
 (Hosanna *2 juu Mbinguni )*2
- Dunia ni ya Bwana na vitu vyote vilivyomo
 Dunia nzima na watu wote waliomo
 Kwa maana yeye ameisimika juu ya bahari
 Akaithibitisha juu ya mito
- Inueni vichwa vyenu, enyi malango
 Inukeni, enyi malango ya kale
 Mfalme wa utukufu apate kuingia
 Ni nani mfalme wa utukufu?
 Bwana mwenye nguvu na uhodari
 Bwana aliye hodari katika vita
- Inueni vichwa vyenu enyi malango
 Inukeni enyi malango ya kale
 Mfalme wa utukufu apate kuingia
 Ni nani mfalme wa utukufu?
 Bwana wa majeshi
 Yeye ndiye mfalme wa utukufu
- Atukuzwe Baba na mwana
 na roho mtakatifu
 Kama mwanzo na sasa na siku zote
 na milele. Amina
 
  
         
                            