Watoto wa Mayahudi

Watoto wa Mayahudi
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Watoto wa Mayahudi Lyrics

Watoto wa Mayahudi walimlaki Bwana
Wakiyachukua matawi ya mizeituni
Wakipiga kelele wakisema
(Hosanna *2 juu Mbinguni )*2

 1. Dunia ni ya Bwana na vitu vyote vilivyomo
  Dunia nzima na watu wote waliomo
  Kwa maana yeye ameisimika juu ya bahari
  Akaithibitisha juu ya mito
 2. Inueni vichwa vyenu, enyi malango
  Inukeni, enyi malango ya kale
  Mfalme wa utukufu apate kuingia
  Ni nani mfalme wa utukufu?
  Bwana mwenye nguvu na uhodari
  Bwana aliye hodari katika vita
 3. Inueni vichwa vyenu enyi malango
  Inukeni enyi malango ya kale
  Mfalme wa utukufu apate kuingia
  Ni nani mfalme wa utukufu?
  Bwana wa majeshi
  Yeye ndiye mfalme wa utukufu
 4. Atukuzwe Baba na mwana
  na roho mtakatifu
  Kama mwanzo na sasa na siku zote
  na milele. Amina