Watu Hawatalingana
Watu Hawatalingana | |
---|---|
Performed by | Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha |
Album | Watu Hawalingani |
Category | Tafakari |
Composer | Fr. A. Msigwa |
Views | 6,279 |
Watu Hawatalingana Lyrics
- {Watu hawatalingana (daima), watatofautiana
(nayo ni) makusudi yake Mungu, jina lake litukuzwe } *3{ Sote tumeumbika tulivyo (kadiri) ya mapenzi yake Mungu
Ili utukufu wake Mungu (Mwenyezi) ujulikane kwa wote } *2 - Kweli wanadamu wote (hakika) tumeumbwa kwa udongo
(hivyo) asili yetu ni moja, tumetoka mavumbini - Wapo walio wanyonge (lakini), pia wapo wenye nguvu
(kusudi) Mungu kawaumba hivyo, ili wahudumiane - Wengine kawabariki (sana), amewajalia mali
(lakini) wengine amewashusha, wamekuwa hohe hahe. - Wale walio tajiri (kamwe), wasiwanyime fukara
(kwani) maskini wahitaji, huruma ya matajiri - Wote tu wana wa Mungu (hivyo) tuonyeshane upendo
(ili) Mungu wetu atukuzwe, sasa na hata milele.
Baadhi ya kwaya ambazo zimerekodi wimbo huu ni
* Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha (Watu Hawalingani album)
* Kwaya ya Mt. Vincenti Palloti Makiungu Dsm (Wema Mkamilifu album)
* Kwaya ya Mt. Paulo, Chuo Kikuu cha Nairobi (Ikatetemeka Nchi album)