Watumishi Wake Baba

Watumishi Wake Baba
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)
VideoWatch on YouTube
Views52,170

Watumishi Wake Baba Lyrics

  1. Watumishi wake Baba wangapi waliopo
    Wanakula na kusaza chakula chake Baba

    Nami - Nami nataabika hapa
    Nashi - Nashiriki na nguruwe
    Chaku - Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi
    Nita - Nitarudi na kusema
    Baba - Baba yangu nisamehe
    Nime - Nimekosa kwake Mungu, na mbele yako Baba

  2. Baba kamwona yu mbali kashikwa na huruma
    Akakimbia kumlaki kamkumbata na busu
  3. Baba sistahili tena kuitwa mwana wako
    Unifanye kama mmoja wa watumishi wako
  4. Baba yangu nimekosa ninaomba huruma
    Unisamehe nirudi nikakutumikie
  5. Wanikaribisha mimi kwenye karamu yako
    Meza imeandaliwa inaningoja mimi
  6. Nasogea ninakuja ninakukimbilia
    Mimi ni mtoto mpotevu Baba unipokee