Wosia
Wosia | |
---|---|
Alt Title | Mkimtumainia Mungu |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Tafakari |
Composer | G. C. Mkude |
Views | 12,482 |
Wosia Lyrics
- Tulieni ndugu zangu niwaambie siri moja
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote
Japo magumu ni mengi mtakayokutana nayo
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote{ Mtavuka vikwazo vya shetani na magumu yote (nasema)
Mbinu zake shetani na hila hazitawaangusha (nasema)
Mkimtumainia Mungu mtayashinda yote } *2 - Kwa nguvu za Mwenyezi nasema hamtaaibika-
Mtautimiza huu wito wenu kikamilifu - - Mungu Baba yuko nyuma yenu anawapigania-
Atawafukuza na maadui wenye hila mbaya . - Wosia ninawapa ndugu muwe na uvumilivu-
Kwani haya ya dunia si kitu wala si lolote .