Yesu Akalia
| Yesu Akalia | |
|---|---|
![]() | |
| Performed by | St. Maurus Kurasini |
| Album | Hubirini Kwa Kuimba |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | G. A. Chavallah |
| Video | Watch on YouTube |
| Views | 14,431 |
Yesu Akalia Lyrics
Yesu akalia kwa sauti kubwa,
{ Akasema,
Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu } *2- Alipokwisha kusema hayo, akakata roho
Yule akida alipoona hayo, akasema
Huyo hakika alikuwa mwana wa Mungu - Na makutano yote ya watu, waloshuhudia
Wakafadhaika wakaenda zao, wakiomba
Wakapigapiga vifua kuomba toba - Na wote waliojuana naye, waloandamana
Wakimfuata toka Galilaya, kwa pamoja,
Wakasimama wakitazama mambo hayo.
