Yesu Mwema Najitolea Kwako
Yesu Mwema Najitolea Kwako | |
---|---|
Performed by | St. Augustine Bugando Mwanza |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | (traditional) |
Views | 22,564 |
Yesu Mwema Najitolea Kwako Lyrics
- Yesu mwema najitolea kwako,
Kwa leo hii na siku zote
Nafsi yangu na moyo wangu wote
Heri kweli, heri kweli, heri kweli raha ya uwingu *2 - Ndani mwangu umekuja daima,
Kuwa nami ni pendo lako
Ewe mpenzi mwenye utamu mwingi
Ni mapendo, ni mapendo, ni mapendo ya moyo wako *2 - Nitaweza kukurudishia nini,
Kwa wema huu na pendo lako
Roho yangu umeifadhilia
Nikupende, nikupende, nikupende ni tamaa yangu*2 - Weka Rabi katika roho yangu,
Wema wako na unyenyekevu,
Na pendo kuu fadhila ya imani
Niongoze, niongoze, niongoze katika imani *2
Harmonized by Fr. Malema