Yesu Mwema Najitolea Kwako

Yesu Mwema Najitolea Kwako
ChoirSt. Augustine Bugando Mwanza
CategoryEkaristia (Eucharist)
Composer(traditional)

Yesu Mwema Najitolea Kwako Lyrics

 1. Yesu mwema najitolea kwako,
  Kwa leo hii na siku zote
  Nafsi yangu na moyo wangu wote
  Heri kweli, heri kweli, heri kweli raha ya uwingu *2
 2. Ndani mwangu umekuja daima,
  Kuwa nami ni pendo lako
  Ewe mpenzi mwenye utamu mwingi
  Ni mapendo, ni mapendo, ni mapendo ya moyo wako *2
 3. Nitaweza kukurudishia nini,
  Kwa wema huu na pendo lako
  Roho yangu umeifadhilia
  Nikupende, nikupende, nikupende ni tamaa yangu*2
 4. Weka Rabi katika roho yangu,
  Wema wako na unyenyekevu,
  Na pendo kuu fadhila ya imani
  Niongoze, niongoze, niongoze katika imani *2