Yesu Nakushukuru
   
    
     
         
          
            Yesu Nakushukuru Lyrics
 
             
            
- Yesu nakushukuru, ( asante ) *4
 { Umenilisha, asante, umeninywesha, asante,
 Umenipenda, asante, umenilinda, asante } *2
- Ee Bwana wangu nitakushukuruje,
 Kwa pendo lako lisilo na kipimo,
 Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,
- Umenitunza kwa msingi wa kweli,
 Naburudika kwa wingi wa divai,
 Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,
- Kwa pendo lako wanilinda salama,
 Kwa wema wako ninapata fanaka,
 Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,
- Ee Yesu wangu nitakushukuruje,
 Kwa ukombozi na zawadi ya mbingu,
 Unanipenda Bwana nasema asante, Bwana,