Yesu wa Vituko
Yesu wa Vituko | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Migori |
Album | Nimeteuliwa |
Category | Kristu Mfalme (Christ the King) |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 11,464 |
Yesu wa Vituko Lyrics
- Huyu ndiye Yesu wa miujiza nauliza
Huyu ndiye Yesu wa maajabu nauliza
Aliyegeuza maji kuwa divai
Kwenye harusi kule Kana GalilayaHuyu ndiye Yesu, (Yesu) Mwana Wa Mungu
Huyu ndiye Yesu, (Yesu) kutoka Mbinguni
Huyu ndiye Yesu, aliyekuja kwetu
Huyu ndiye Yesu mwenye upendo mwingi - Huyu ndiye Yesu Mnazareti nauliza
Huyu ndiye Mwana wa seremala nauliza
Aliyewaita wavuvi wa samaki
Akawageuza wavuvi wa watu - Huyu ndiye Yesu mwenye huruma nauliza
Huyu ndiye Yesu Simba wa Yuda nauliza
Aliyewakemea mapepo kwa nguvu
Aliyewaamuru mapepo watoke - Huyu ndiye Yesu mwenye baraka nauliza
Huyu ndiye Yesu mwenye chakula nauliza
Aliyewalisha watu elfu tano
Kwa mikate mitano na samaki wawili - Huyu ndiye Yesu mwenye vituko nauliza
Huyu ndiye Yesu asiyeshindwa nauliza
Aliyewatimua watu hekaluni
Walipogeuza hekalu kuwa soko - Huyu ndiye Yesu mwenye hekima nauliza
Huyu ndiye Yesu mwenye elimu nauliza
Aliyeng'amua hila zake shetani
Pale nyikani alipojaribiwa