Yesu wa Vituko

Yesu wa Vituko
ChoirSt. Joseph Migori
AlbumNimeteuliwa
CategoryKristu Mfalme (Christ the King)
ComposerAlfred Ossonga

Yesu wa Vituko Lyrics

 1. Huyu ndiye Yesu wa miujiza nauliza
  Huyu ndiye Yesu wa maajabu nauliza
  Aliyegeuza maji kuwa divai
  Kwenye harusi kule Kana Galilaya

  Huyu ndiye Yesu, (Yesu) Mwana Wa Mungu
  Huyu ndiye Yesu, (Yesu) kutoka Mbinguni
  Huyu ndiye Yesu, aliyekuja kwetu
  Huyu ndiye Yesu mwenye upendo mwingi

 2. Huyu ndiye Yesu Mnazareti nauliza
  Huyu ndiye Mwana wa seremala nauliza
  Aliyewaita wavuvi wa samaki
  Akawageuza wavuvi wa watu
 3. Huyu ndiye Yesu mwenye huruma nauliza
  Huyu ndiye Yesu Simba wa Yuda nauliza
  Aliyewakemea mapepo kwa nguvu
  Aliyewaamuru mapepo watoke
 4. Huyu ndiye Yesu mwenye baraka nauliza
  Huyu ndiye Yesu mwenye chakula nauliza
  Aliyewalisha watu elfu tano
  Kwa mikate mitano na samaki wawili
 5. Huyu ndiye Yesu mwenye vituko nauliza
  Huyu ndiye Yesu asiyeshindwa nauliza
  Aliyewatimua watu hekaluni
  Walipogeuza hekalu kuwa soko
 6. Huyu ndiye Yesu mwenye hekima nauliza
  Huyu ndiye Yesu mwenye elimu nauliza
  Aliyeng'amua hila zake shetani
  Pale nyikani alipojaribiwa