Zawadi Tosha
Zawadi Tosha | |
---|---|
Performed by | St. Francis of Assisi Kariobangi |
Album | Zawadi Tosha |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Views | 18,493 |
Zawadi Tosha Lyrics
Nimetunukiwa tuzo lenye thamani
Nimeletewa zawadi toka mbinguni
Nimejishindia Mwana wa Mungu
Nimepewa Yesu zawadi tosha- Ninashangilia naimba kwa furaha
Ninarukaruka nacheza kwa furaha
Napiga makofi na vigelegele
Nimempata Yesu tuzo la ajabu (mimi) - Ninakushukuru ee Mungu Baba yetu
Nasema asante kwa mema yako yote
Napiga filimbi, ngoma na kayamba
Nimejishindia Bwana wa mabwana - Nikiwa na Yesu, magonjwa yamepona
Nikiwa na Yesu mashaka yamekwisha
Yesu kiongozi, Yesu Jemedari
Yesu mchungaji, Yesu mambo yote - Maisha marefu ni tuzo nimetuzwa
Uzima milele nimeshaahidiwa
Mbinguni kwa Baba nitakaribishwa
Nitaishi vyema siku zangu zote