Zungukazunguka

Zungukazunguka
Alt TitleMbinguni Kwa Baba
ChoirSt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryTafakari
ComposerAlfred Ossonga

Zungukazunguka Lyrics

 1. Mbinguni kwa Baba, kweli kuna raha,
  Makerubi wote hata maserafi
  Malaika wote na watakatifu,
  Wako mbele za Mungu kila mtu na kazi yake

  Waimbaji tutaimbaimba, tutaimba nyimbo za shangwe
  Malaika watarukaruka, wataruka mbele za Mungu
  Watu wote (kweli) watafurahi nyumbani mwa Bwana
  Watacheza (wote) pamoja wakizungukazunguka

 2. Tuimbe nyimbo nzuri kama makerubi,
  Tuimbe kwa furaha kama maserafi
  Na tuchezecheze kama watakatifu,
  Tukirukaruka kama malaika wa Mungu
 3. Wenye moyo safi na matendo mema,
  Twendeni kwa Baba tupate dhawabu
  Tumekaribishwa Mbinguni kwa Baba
  Twendeni tuone, jinsi tulivyoandaliwa.
 4. Sisi tunaimba nyimbo za Mbinguni,
  Tena twatabiri yale ya Mbinguni
  Yote yalopita kwa wenye hekima,
  Tumefunuliwa, tutangaze kwa nyimbo hizi
 5. Fanya utafiti na upeleleze,
  Utafunuliwa siri za Mbinguni
  Waloshinda vita, wateule wa Mungu
  Wanatungojea kwenye raha ya siku zote