Kumekucha Lyrics

KUMEKUCHA

@ Bernard Mukasa

Kumekucha - ni siku kubwa ya ajabu leo hii
Kumekucha - ni siku ya furaha na amani
{ Watu wote - wanameremeta, tazama
Wamevaa - mavazi mazuri oneni
Nyuso zao - tabasamu shangwe nderemo na vifijo } *2

 1. [ s ] Pokeeni bahati yenye upekee
  Kufurahiya pendo lisilo dosari
  La mwenyezi Mungu mwema na mkari-mu
 2. Heri gani ndugu tumejaliwa leo
  Kusimama pamoja tukiwa na hamu
  Kuyashuhudia makuu ya le-o
 3. Tupaze sauti wote watusikie
  Watakaoweza wajumuike nasi
  Shangwe nderemo chereko na vifi-jo
Kumekucha
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Don Bosco Mirerani
ALBUMIkulu ya Mbinguni
CATEGORYEntrance / Mwanzo
MUSIC KEYKey G Major 2/4
TIME SIGNATURE2
4
 • Comments