Majukumu Katika Familia
Majukumu Katika Familia |
---|
Alt Title | Baba Mama na Watoto |
Performed by | St. Don Bosco Mirerani |
Album | Ikulu ya Mbinguni |
Category | Familia |
Composer | T. B. Pamera |
Views | 9,689 |
Majukumu Katika Familia Lyrics
Baba mama na watoto wao ni familia kamili
Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake
Mama awe katekista, na baba awe padre
Mama awe katekista, na baba awe padre
{Watoto wawe ubao[ubao] kufundishia wengine
Ili wengineo wajifunze, kuishi maisha mema} *2
- Mama awe katekista maana yeye ndiye mwalimu[yeye],
Kwa kuwa ana huruma[sana] na ni mlezi wa watoto
Awafundishe mema yote, upendo sala na bidii[ya kazi]
Na kuwafundisha nidhamu kwa wenyewe na kwa wengine
- Baba yeye awe padre, tena yeye ndiye mchungaji[mwema]
Ashirikiane naye mama, watoto wao kuwalea
Awe mwelekezaji pale watoto wanapopotoka [warudishwe]
Ili waweze kujenga familia iliyo bora
- Watoto wawe ubao ubao, kufundishia wengine[waige]
Kwa tabia zao nzuri na uadilifu mwema
Watakuwa ni mfano bora na kielelezo sawia [cha kuigwa]
Hiyo ndiyo familia ya kumpendeza Mungu
Baba mama na watoto wao ni familia kamili
Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake