Baba Mama na Watoto
Baba Mama na Watoto | |
---|---|
Performed by | St. Cecilia Zimmerman |
Album | Nitayasimulia Matendo (Vol 6) |
Category | Familia |
Composer | T. B. Pamera |
Views | 10,021 |
Baba Mama na Watoto Lyrics
- Baba mama na watoto wao ni familia kamili
Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
Na kupeana majukumu, kila mmoja na lakeMama awe katekista, na baba awe padre
Mama awe katekista, na baba awe padre
{Watoto wawe ubao[ubao] kufundishia wengine
Ili wengineo wajifunze, kuishi maisha mema} *2 - Mama awe katekista maana yeye ndiye mwalimu
Kwa kuwa ana huruma na ni mlezi wa watoto
Awafundishe mema yote, upendo sala na bidii
Na kuwafundisha nidhamu kwa wenyewe na kwa wengine - Baba yeye awe padre, tena yeye ndiye mchungaji
Ashirikiane naye mama, watoto wao kuwalea
Awe mwelekezaji pale watoto wanapopotoka
Ili waweze kujenga familia iliyo bora - Watoto wawe ubao ubao, kufundishia wengine
Kwa tabia zao nzuri na uadilifu mwema
Watakuwa ni mfano bora na kielelezo sawia
Hiyo ndiyo familia ya kumpendeza Mungu
Baba mama na watoto wao ni familia kamili
Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake