Tumeuona Wema
| Tumeuona Wema | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha | 
| Album | Kidole Juu (Vol 23) | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Composer | F. Mwaluko | 
| Views | 10,386 | 
Tumeuona Wema Lyrics
- Tumeuona wema wako Bwana Mungu
 Tumeuona wema wako Mungu wetu
 Umetuonyesha mapito yenye haki
 Tumeelewa na kufafanua mema
 Ni wema - wa ajabu, ni pendo - pendo kuu
 (Pokea) Pokea sifa na shukrani zangu }*2
- Ni wewe Bwana watupenda
 watujalia mema mengi
 Sifa na utukufu wake vimedhihirihswa
 Bwana tunakushukuru
- Na malaika wanaimba kusifu utukufu wako
 Furaha imetanda kote furaha ya kweli
 Bwana twakushangilia
- Viumbe vyote vyakusifu, vyashangilia kwa furaha
 Ni wewe Bwana ulinena navyo vikaumbwa
 Bwana wastahili sifa
 
  
         
                            