Tukeshe
| Tukeshe | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Kidole Juu (Vol 23) |
| Category | Tafakari |
| Composer | P. F. Mwarabu |
| Views | 7,503 |
Tukeshe Lyrics
Tukeshe - Tukeshe sote kila wakati
Tukimwomba Mungu atupe Baraka zake
Tukeshe - Tukeshe tukeshe kila wakati
Tukimwomba Yesu atufikishe Mbinguni- [s] Na tukeshe kama wale wanawali
Waliozijaza taa zao mafuta - [t] Tukeshe tukiomba kwa moyo wote
Tuupate uzima wa milele - Watu wote tukeshe siku zote
Tuziweke hazina mbinguni
Siku ya mwisho tufike kwake Mungu
Tuishi naye milele milele - Dunia hii ni shida na mateso
Tusidanganywe na raha za muda
Ona dhambi maovu na magonjwa
Yanatisha tena yahuzunisha - Tujikane tutubu tuungame
Tujaliwe huruma yake Mungu
Tusali sana tuombe neema zake
Tuwe tayari siku ya hukumu