Mwimbieni Bwana Zaburi
Mwimbieni Bwana Zaburi | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Kidole Juu (Vol 23) |
Category | Entrance / Mwanzo |
Composer | G. Tesha |
Views | 6,990 |
Mwimbieni Bwana Zaburi Lyrics
Mwimbieni Bwana zaburi
Mwimbieni kwa kinubi) *2
{Mwimbieni kwa kinubi na sauti ya zaburi
Mwimbieni kwa panda na sauti ya baragumu (wote)
Shangilieni mbele za mfalme Bwana wa majeshi}- Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu na wote wanaokaa ndani yake
Milima naiimbe kwa furaha mbele za Bwana Mungu - Wanyama wa mwituni na mimea ya kondeni
Upepo na uvume kupeleka habari hizi
Kwa ndege wa angani na viumbe vilivyo baharini - Nikitazama kushoto kulia nyuma na mbele
Nikitazama angani nikitazama ardhini
Kila nionacho kinasimulia utukufu wako - Kwa maana mbingu na dunia ni kazi yako
Jua na mwezi na nyota anga pia nayo mawingu
Ni kazi ya vidole vyako na ujuzi wa mikono yako