Login | Register

Sauti za Kuimba

Mwimbieni Bwana Zaburi Lyrics

MWIMBIENI BWANA ZABURI

@ G. Tesha

Mwimbieni Bwana zaburi
Mwimbieni kwa kinubi) *2
{Mwimbieni kwa kinubi na sauti ya zaburi
Mwimbieni kwa panda na sauti ya baragumu (wote)
Shangilieni mbele za mfalme Bwana wa majeshi}

 1. Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
  Ulimwengu na wote wanaokaa ndani yake
  Milima naiimbe kwa furaha mbele za Bwana Mungu
 2. Wanyama wa mwituni na mimea ya kondeni
  Upepo na uvume kupeleka habari hizi
  Kwa ndege wa angani na viumbe vilivyo baharini
 3. Nikitazama kushoto kulia nyuma na mbele
  Nikitazama angani nikitazama ardhini
  Kila nionacho kinasimulia utukufu wako
 4. Kwa maana mbingu na dunia ni kazi yako
  Jua na mwezi na nyota anga pia nayo mawingu
  Ni kazi ya vidole vyako na ujuzi wa mikono yako
Mwimbieni Bwana Zaburi
COMPOSERG. Tesha
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMKidole Juu (Vol 23)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
REFPs. 98
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments