Mungu ni Mmoja
Mungu ni Mmoja | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Kidole Juu (Vol 23) |
Category | TBA |
Composer | G. C. Mkude |
Views | 15,143 |
Mungu ni Mmoja Lyrics
Amka asubuhi tembeeni mchana pia usiku mpumzike
Fanyeni kazi zenu na pia mtambue
Yupo anayewezesha hayo (kwa kweli)
Ni mmoja tu, ni mmoja tu, ni mmoja yeye ni mmoja tu
Ni Mungu Baba yetu anayewezesha yote.- Yeye anajua mapito yetu tulalapo hata tuamkapo
Sifa heshima tumpeni Mungu aliyetuumba - Yeye ndiye Mungu wa baba zetu katuwezesha kuyapata yote
Sifa heshima tumpeni Mungu aliyetuumba - Na tumtambue tumheshimu tupige magoti mbele za Bwana
Sifa heshima tumpeni Mungu aliyetuumba