Asante Kwa Wema
| Asante Kwa Wema | |
|---|---|
| Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
| Album | Kidole Juu (Vol 23) |
| Category | Thanksgiving / Shukrani |
| Composer | Single |
| Views | 20,866 |
Asante Kwa Wema Lyrics
- Bwana alinitendea mambo makuu
Nilipoita jina lake aliniitikia
Alinitegemeza katika taabu zangu{ Asante- kwa wema wako
Asante-kwa ukarimu
Asante kwa pendo lako nashukuru } * 2 - Bwana ameniponya na magonjwa mengi
Pia amenikinga na ajali mbaya sana
Amenitoa katika mitego ya shetani - Nimetafakari upendo wake Bwana
Kujivika ubinadamu na kufa msalabani
Ili nikombolewe utumwani wa shetani - Ni mara nyingi sana nimetenda dhambi
Lakini Bwana Yesu hakunihukumu kwa dhambi
Hakuna kama Bwana yeye ni Mungu pekee - Wema wake Mungu wangu hauna mwisho
Ameniandalia makao baada ya kifo
Masharti yake niwe nimetii amri za Mungu - Enyi ndugu zangu mlio katika Kristu
Unganeni pamoja nami kumshukuru Mungu
Ni mema mengi sana yeye ametujalia