Tutalihubirije Neno
Tutalihubirije Neno Lyrics
Tutalihubirije neno lake Mungu
Huku viunoni mwetu ni mahirizi
Neno la Mungu halifanyiwi dhihaka
Tukaeni tukilijua jambo hili
Tuzitoe hirizi viunoni mwetu
Na vibuyu vilivyomo ndani ya nyumba
Tuuteketezeni ufalme wa giza
Tuukaribishe ufalme wa Mbinguni
Sikieni niwaambie siri moja
Ushirikina mwisho wake jehanamu
Tukikabidhi maisha yetu kwa Mungu
Tutapata mema na raha ya mbinguni
- Ukitazama baadhi ya familia
Waziamini tunguri kuliko Mungu
Ukitazama baadhi ya familia
Wanaendesha kazi zao kwa tunguri
- Wakati wengine wanapoenda ibada
Sisi wengine tunakwenda kunywa pombe
Kutokana na malezi yao nyumbani
Na watoto disko kulisakata rumba
- Ndugu zangu sasa ninawakaribisha
Tuingie ndani ya hekalu ya Mungu
Kabidhi kila kitu kwake Mungu Baba
Mungu Baba ndiye mwisho wa mambo yote