Ingawa Napendeza

Ingawa Napendeza
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumMaajabu ya Mungu
CategoryTafakari
ComposerGerdian Rweikiza
Views4,573

Ingawa Napendeza Lyrics

  1. Ingawa mimi napendeza, Ingawa wewe wapendeza
    Wapendeza machoni pa watu, kupendeza si kitu
    Ingawa mimi najipamba, Ingawa wewe wajipamba
    Kujipamba kwa mwili si kitu, kujipamba si kitu

    Kujipamba kwa imani bila matendo ni bure
    Wajidanganya tu
    Kujipamba kwa mavazi bila matendo ni bure
    Twajidanganya tu

    Uzuri wa uso wako - bila Mungu ni bure
    Wingi wa mali yako - bila Mungu ni bure
    Uzuri watoka kwa Mungu, mali yatoka kwa Mungu
    Na majivuno yote, bila Mungu ni bure
    Kumbuka kila mtu, kaumbwa kwa jinsiye

  2. Wengi wajisifia kwa maneno ya watu
    Wanapakwa kila kona kwa maneno mazuri
    Bila kufikiria na wewe wajiona mzuri
    Mpaka kufikia kusahau maagano yake
    Kwa kusifiwasifiwa
  3. Uzuri ulio nao mshukuru Mungu
    Mali uliyo nayo mshukuru Mungu
    Uzuri ni talanta toka kwa Mungu
    Tumia uzuri wako kumshukuru Mwenyezi