Kulea Watoto

Kulea Watoto
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumMaajabu ya Mungu
CategoryFamilia
ComposerS. Z. Mutafungwa
Views5,614

Kulea Watoto Lyrics

TUWAOKOE WATOTO

  1. Kulea watoto ni kazi ya baba na kazi ya mama
    Hilo ndilo jukumu walilopewa na Mwenyezi Mungu
    Na kazi hiyo ifanywe kwa msaada wake Muumba

    Ni kwa nini tunawanyima malezi bora na ya muhimu?
    Ni kwa nini tunawabembeleza watoto manyumbani?

    {Watoto wanahitaji malezi yaliyo mema
    Ni lazima waonyeshwe njia bora ya kupita
    Ili kuwafurahisha wazazi na baadaye taifa}*2

  2. Angalia watoto wadogo wanavyozurura
    Usiku kucha utafikiri kwao ni mchana
    Waone watoto wanavyofaa wengine nusu uchi
    Mbele ya jamii pia na kwa wazazi wao
  3. Mtoto anahitaji kupata angali mbichi
    Ili aweze kukua katika maadili mema
    Wazazi acheni pia kuwalea watoto kitajiri
    Na kuwapa pesa nyingi eti ni za matumizi
  4. Pesa za watoto zinaishia kununua bangi
    Kununulia kila aina ya dawa za kulevya
    Tunadhani tunawapenda watoto kumbe tunawaharibu
    Tujirekebishe wazazi tuokoe watoto