Kulea Watoto Lyrics

KULEA WATOTO

@ S. Z. Mutafungwa

TUWAOKOE WATOTO

Kulea watoto ni kazi ya baba na kazi ya mama
Hilo ndilo jukumu walilopewa na Mwenyezi Mungu
Na kazi hiyo ifanywe kwa msaada wake Muumba

Ni kwa nini tunawanyima malezi bora na ya muhimu?
Ni kwa nini tunawabembeleza watoto manyumbani?

{Watoto wanahitaji malezi yaliyo mema
Ni lazima waonyeshwe njia bora ya kupita
Ili kuwafurahisha wazazi na baadaye taifa}*2

 1. Angalia watoto wadogo wanavyozurura
  Usiku kucha utafikiri kwao ni mchana
  Waone watoto wanavyofaa wengine nusu uchi
  Mbele ya jamii pia na kwa wazazi wao
 2. Mtoto anahitaji kupata angali mbichi
  Ili aweze kukua katika maadili mema
  Wazazi acheni pia kuwalea watoto kitajiri
  Na kuwapa pesa nyingi eti ni za matumizi
 3. Pesa za watoto zinaishia kununua bangi
  Kununulia kila aina ya dawa za kulevya
  Tunadhani tunawapenda watoto kumbe tunawaharibu
  Tujirekebishe wazazi tuokoe watoto
Kulea Watoto
COMPOSERS. Z. Mutafungwa
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMaajabu ya Mungu
CATEGORYFamilia
 • Comments