Nyota ya Bahari
Nyota ya Bahari | |
---|---|
Performed by | Our Lady(Star of the Sea) Kenya Navy |
Album | Tumeandamana |
Category | Bikira Maria |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 13,581 |
Nyota ya Bahari Lyrics
- Bara na bahari furahini sana
Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni
Bara na bahari furahini sana
Tumemulikwa na nuru ya MbinguniTumemulikwa na nyota ya bahari
Bikira daima (mulika) mulika nyoyo zetu
Tumeona leo mwangaza wa kweli
Somo wa kanisa (mulika) mulika njia zetu
{(Mama) Mama tuombee, mama tuongoze
Kwa mwanao Yesu, kule uwinguni } *2 - Pendo lako mama, limetuvutia
Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo
Bara shangilia, bahari ivume
Tumsifu mama, mama wa Maulana - Piga tarumbeta, pigeni mluzi
Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu
Chezeni pamoja, ruka juu juu
Mama wa Yesu afurahi Mbinguni - Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu
Mwanga anamu somo wa kwaya yetu
Uliyekingiwa dhambi ya asili
Daraja letu tuendao Mbinguni - Nyota za angani zamulika nchi
Mama Maria anamulika nyoyo
Usiku mchana anatuangaza
Tunatembea na nuru siku zote