Johera
   
    
     
         
          
            Johera Lyrics
 
             
            
- Johera ( dakunyi's herahera)*2
 Manyase endwaro wololo hawawene
 Johida (dakunyi's hidahida )*2
 Manyase endwarowololo niwakadhi
 Njooni wote tushangilie,
 {Tuimbe kwa furaha, tucheze bila mwisho,
 Tutoe shukrani kwa Bwana mtawala }*2
- Waumini simameni, mbele zake Mungu wetu
 Waimbaji mziimbe, sifa zake Jehova Rama
 Waumini tamkeni, utukufu wake Yahweh
 Makasisi na watawa na wacheze nyumbani mwake
 shangwe
- Kwa sauti ya kinanda, kwa filimbi na kayamba
 Kwa kinubi na kwa zeze, tunamwimbia Mungu wetu
 Kwa kelele za furaha, kwa makofi kwa machezo
 Kwa vigelegele kweli, njooni nyote tutoe shukrani
- Mwimbieni Mungu wetu, mwimbieni wimbo mpya
 Mwimbieni kwa furaha mwimbieni kwa shangwe kubwa
 Mungu wetu ni mkuu, ametenda maajabu
 Ameumba vitu vyote, ulimwengu na jeshi lake lote
- Mungu wetu katuumba, ili sote tumjue
 Sisi sote tumpende, tumtumikie daima
 Ametupa vitu vyote,atulinda siku zote
 Tuna heri ya milele, tutaishi mbinguni kwake Baba