Waumini Simameni
Waumini Simameni Lyrics
- Waumini simameni - tupeleke neno lake
Neno lake Bwana Mungu - ni nuru ya ulimwengu *2
Tulisome kweli (kweli kweli)
Tulihubiri sana(biri sana)
Tulisambaze kote na tulifundishe kweli
Tulisome kweli (kweli kweli)
Tulihubiri sana(biri sana)
Tulisambaze kote na tulifundishe
- Ni neno la Bibilia - kutoka kwa Mungu Baba
Anena kwa kinywa chake - na kwa maandiko yake *2
- Ni dawa ya mioyo yetu - tulizo kwa watu wote
Tulipokeeni leo - tupate kunusurika *2
- Tuchezeni kwa furaha - nderemo na kwa vifijo
Kwa ngoma na tarumbeta - kayamba hata vinanda
- Milima iyumbeyumbe - miti na ichezecheze
Bahari ivume sana - mito ipige makofi *2