Katika Taabu

Katika Taabu
Performed bySt. Mary's Ongata Rongai
AlbumYesu Nakushukuru
CategoryZaburi
ComposerOchieng Odongo
Views4,772

Katika Taabu Lyrics

  1. {/s/: Ee Bwana wangu ninakuomba
    /w/: Bwana uwe pamoja nami }*2
    {(Kweli) katika taabu (tabu) zangu zote
    (Bwana) Katika taabu zangu zote }*2

  2. Aketiye mahali pa siri pake
    Atakaa katika uvuli wake
    Nitasema Bwana ndiye kimbilio
    Ngome yangu nitakayemtumaini
  3. Mabaya hayatakupata mwenzangu
    Tauni haitakaribia kwako
    Kwani atakuagizia malaika
    Wakulinde katika njia zako zote
  4. Mikononi mwao watakuchukua
    Usije ukajikwaa kwenye jiwe
    Utawakanyaga simba pia nyoka
    Wala simba na nyoka utawaseta
  5. Kwa kuwa amenijua jina langu
    Taniita nami nitamwitikia
    Nitakuwa pamoja naye taabuni
    Nitamuokoa na kumtukuza