Katika Taabu
   
    
     
         
          
            Katika Taabu Lyrics
 
             
            
- {/s/: Ee Bwana wangu ninakuomba
 /w/: Bwana uwe pamoja nami }*2
 {(Kweli) katika taabu (tabu) zangu zote
 (Bwana) Katika taabu zangu zote }*2
- Aketiye mahali pa siri pake
 Atakaa katika uvuli wake
 Nitasema Bwana ndiye kimbilio
 Ngome yangu nitakayemtumaini
- Mabaya hayatakupata mwenzangu
 Tauni haitakaribia kwako
 Kwani atakuagizia malaika
 Wakulinde katika njia zako zote
- Mikononi mwao watakuchukua
 Usije ukajikwaa kwenye jiwe
 Utawakanyaga simba pia nyoka
 Wala simba na nyoka utawaseta
- Kwa kuwa amenijua jina langu
 Taniita nami nitamwitikia
 Nitakuwa pamoja naye taabuni
 Nitamuokoa na kumtukuza