Uje Roho Mtakatifu

Uje Roho Mtakatifu
Performed bySt. Mary's Ongata Rongai
AlbumYesu Nakushukuru
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)
ComposerOchieng Odongo
Views8,846

Uje Roho Mtakatifu Lyrics

  1. {Uje Roho Mtakatifu njoo (njoo)
    Uziendee roho za waumini }*2
    {(Wote) Uwajalie mapendo yako alleluia
    (Kweli) Uje Roho Mtakatifu (kweli) uje mfariji }*2

  2. Roho ya Bwana imeujaza ulimwengu
    Nayo inayoviunganisha viumbe vyote
    Hujua maana kila sauti alleluia
  3. Neno la Bwana hakika limeshaaminiwa
    Katika mioyo yetu sisi waamini
    Na roho mtakatifu tuliopewa alleluia
  4. Roho yule aliyewashukia mitume
    Waliokuwa wamekusanyika pamoja
    Nasi tutajazwa na Roho kweli alleluia
  5. Mungu Mwenyezi alituumba sisi sote
    Na Mungu Mwana akatukomboa kwa damu
    Na Mungu Roho anatulinda sisi siku zote