Tembea na Yesu Lyrics

TEMBEA NA YESU

@ Ochieng Odongo

Tembea, ndugu yangu -
Tembea na Yesu (kwa hakika)
Tembea, siku zote -
Tembea na Yesu (kweli) *2

 1. Ukiwa safarini, hata uwe nyumbani
  Ukiwa kanisani, na hata uwe kazini
 2. Ukienda safari, ukienda shuleni
  Shida zinapokuja, hata ukifanikiwa
 3. Ukiwa na magonjwa, hata uwe na afya,
  Ukiwa maskini, na hata uwe tajiri
 4. Vita vinapokuja, amani isiwepo
  Ukiwa na huzuni, hata uwe na faraja
Tembea na Yesu
COMPOSEROchieng Odongo
CHOIRSt. Mary's Ongata Rongai
ALBUMYesu Nakushukuru
CATEGORYTafakari
 • Comments