Kama Vile Mwili

Kama Vile Mwili
Performed bySt. Mary's Ongata Rongai
AlbumYesu Nakushukuru
CategoryChurch
ComposerOchieng Odongo
Views3,730

Kama Vile Mwili Lyrics

  1. {Kama vile mwili ni mmoja nao unao viungo vingi
    Tena na viungo vyote vya mwili ulonavyo ni vingi
    (Kweli) Ni mwili mmoja }*2
    {Vinafanya kazi zote, kwa pamoja siku zote
    Kwani vyote vya maana, na vizuri kwelikweli
    Nasi sote Wakristu tushirikiane }*2

  2. Kwa maana katika Roho, sisi sote tulibatizwa
    Tulinyweshwa Roho mmoja, basi sote ni mwili mmoja
  3. Kama sisi ni Wayahudi au sisi ni Wayunani
    Tukiwa ndani ya Yesu hatuko tofauti kabisa
  4. Miguu, mikono na macho masikio hata mapua
    Na viungo vyote vya mwili vinafanya kazi kwa pamoja
  5. Katika kanisa la Bwana sisi sote tuna nafasi
    Tutumie nafasi zetu kwa huduma ya kanisa lake