Ndiwe Kuhani
Ndiwe Kuhani Lyrics
{/b/: Ndiwe kuhani hata milele (wewe)
/w/: Ndiwe kuhani hata milele}*2
{Kwa mfano wake - Melekizedeki (kweli)
Kwa mfano wake Melekizedeki }*2
- Neno la Bwana kwa bwana wangu
Uketi mkono wa kuume
Mkono wake Mungu Mwenyezi
- Niwafanyapo adui zako
Kuachilia miguu yako
Watajikwaa na kuanguka
- Akainyoosha nyoka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako ee Bwana
Kuishi kati ya adui zako
- Uzuri wa utakatifu
Tokea tumbo la asubuhi
Pokea umande wa ujana wako
- Bwana ameapa siku zote
Wata hataghairi kabisa
Ndiwe kuhani hata milele